Historia ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania inaanzia tarehe 19 machi 1926 siku ambayo bunge la uingereza lilipitisha sheria iliyoitwa "The Tanganyika (legislative council) order in 1926".
Tanganyika wakati huo ilikua chini ya utawala wa muingerezaambayo ilikuwa imepewa mamlaka na umoja wa mataifa kuisimamia
Tanganyika hadi ipate uhuru wake. Sheria hiyo ambayo ilitaka kuanzishwa Baraza la Kutunga Sheria nchini, ilichapishwa katika gazeti la serikali tarehe 18 juni 1926. Baraza hilo liliitwa "The Council of Tanganyika territory" na kujulikana zaidi kwa kifupi kama "LEGCO". Baraza hili lilizinduliwa tarehe 7 Desemba 1926 mjini Dar es salaam chini ya uwenyekiti wa Sir. Donald Cameron likiwa na wajumbe 20 wote wakiwa wameteuliwa na Gavana. Sheria zote zilizokua zikitungwa na Baraza hili zilikuwa zinapelekwa Uingereza kwa ajili ya kupata idhini ya Mkuu wa Nchi kabla ya kuanza kutumika.
Mabadiliko Mbali Mbali
Mabadiliko makubwa ya kwanza kufanyika katika baraza la kutunga sheria yalikua mwaka 1953 wakati Gavana alipoondolewa kuongoza na nafasi yake kuchukuliwa na spika. Brigadier William Erick Halstead Sculpham, aliapishwa tarehe 1 Novemba 1953 kuwa spika wa kwanza wa Baraza. Aidha, utaratibu ulibadilika kwa sheria zilizotungwa na Baraza kuanza kuidhinishwa na Gavana kwa niaba ya Mfalme/Malkia wa Uingereza.
Mabadiliko makubwa ya pili yalikuwa mwaka 1958 ambapo kwa mara ya kwanza Baraza lilipata wajumbe wa kuchaguliwa na watu. katika uchaguzi uliofanyika mwaka huo, vyama vitatu vya siasa vilishiriki ambavyo ni;-
- Tanganyika African National Union (TANU)
- United Tanganyika Party (UTP)
- African National Congress (ANC).
Mabadiliko makubwa ya tatu yalitokea mwaka 1960 kwenye uchaguzi wa pili ambao ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya uhuru wa Tanganyika ambapo wajumbe wote walichaguliwa. Aidha, jina la chombo hiki lilibadilika kutoka kuwa Baraza la Kutunga Sheria na kuwa Bunge (National Assembly) Lengo lilikua ni kuandaa mfumo ili baada ya uhuru Rais wa Tanganyika awe na mamlaka kikatiba ya kutoa idhini kwa sheria zinazotungwa na Bunge.
Baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, pamekuwa na mabadiliko mengine makubwa matatu mabayo ni
- Bunge kuwa na sura ya muungano mwaka 1964.
- Bunge kuwa la chama kimoja mwaka 1965
- Na kurejeshwa kuwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992 ambao ulilifanya bunge kuwa la vyama vingi kuanzia uchaguzi mkuu wa mwaka 1995.
KUMBI ZILIZOWAHI KUTUMIKA NA BUNGE
Baraza la kutunga sheria lilikuwa likifanyia vikao vyake kwenye ukumbi wa ANATOUGLOU na baadaye kuhamia jengo ambalo siku hizi linaitwa FREE MASON HALL. Baada ya hapo bunge likawa likikutana katika ukumbi wa KARIMJEE mjini Dar es salaam. Mapema miaka ya themanini, mikutano midogo ya bunge ilianza kufanyika kwenye ukumbi wa CCM Dodoma huku Mkutano wa Bajeti ukiendelea kufanyikia karimjee Dar es salaam. Utaratibu huu uliendelea hadi mwishoni mwa miaka ya tisini ndipo bunge lilipoanza kufanya mikutano yake yote Dodoma kwenye ukumbi wa PIUS MSEKWA
Ukumbi wa sasa wa bunge
- Majukwaa mawili kwaajili ya wananchi (Public Galleries) wanaopata fursa ya kushuhudia vikao vya bunge. Majukwaa haya yanauwezo wa kuchukua wageni 84 kila moja.
- Jukwaa maalum la wageni wa spika ( Speaker's Gallery). Eneo hili ni kwa ajili ya wageni mashuhuri na wageni wengine wa spika na lina uwezo wa kuchukua watu 40 waliokaa.
- Majukwaa matatu kwa ajili ya maafisa wa serikali kutoka wizara mbali mbali (Government Officials Galleries) wanaokuja bungeni. maeneo haya yana uwezo wa kuchuku watu 25 kila moja
- Jukwaa moja kwa ajili ya waandishi wa Habari (Presss Gallery) ambao huripoti habari za bunge wakati wa mikutano ya Bunge. Eneo hili linauwezo wa kuchukua watu 25.
No comments:
Post a Comment